Sw.tek

@teknolojia
3 Followers
11 Following
196 Posts
Twitterwww.twitter.com/swahili_tek

🆕 Bluesky imezidi kupata watumiaji wengi baada ya Elon kuamua X/Twitter isiwe na uwezo wa ku-block post za mtu.

Bluesky imepata watumiaji wapya 700,000 ndani ya wiki moja. Sasa mtandao huu una watumiaji Milioni 14.5

🆕 Roboti msanii Ai-Da ameweka historia kuuza picha ya Alan Turing kwa dola milioni 1.08!

Sanaa hii ya kipekee inawakilisha changamoto na maswali kuhusu mustakabali wa AI, imetengenezwa na roboti ambaye ameichora kwa mikono yake.

🆕 SpaceX inapanga kufanya jaribio la kujaza mafuta baina ya Starship mbili zikiwa kwenye obiti nje ya anga la dunia, ambapo chombo cha kwanza kitazinduliwa kwenda kwenye obiti ya chini ya Dunia mwezi Machi 2025.

Jaribio hili litakuwa la kwanza kuhamisha mafuta nje ya anga

🍕💰 Mwaka 1994, Chris Clark alinunua domain pizza.com kwa matumaini ya kuvutia kampuni ya pizza. Hakupata mafanikio, lakini akaendelea kulipia gharama ya domain kila mwaka.

Mwaka 2008, aliuza domain ya pizza.com kwa dola milioni 2.6!

🆕 Apple imefanya mabadiliko ya icons za iPhone, mfumo mpya wa iOS 18.2

Mwonekano mpya utakuwa na icon za Settings ambazo zinabadilika rangi.

🔥 Huyu jamaa amevuma mtandaoni.

Alijikuta amepanda ndege ambayo haina abiria wengine, akapiga picha katika kila kiti na kisha akaunganisha kwa kutumia photoshop.

Hii picha imeenda viral 🤣

Diski ya 10MB - miaka ya 1960’s

🚨 Unakuta umekaa zako kimya, upo busy na mishe zako, anatokea mtu pembeni anaangaalia video mitandaoni kwa sauti kubwa na kuondoa ukimya kwenye eneo.

Tabia hii kiukweli inakuwa sio poa kabisa. Watu wanatakiwa kujifunza kuangalia mitandao kwa ukimya bila kusumbua watu wengine.

📊 Nvidia imeendelea kupanda thamani yake kwenye soko la hisa, na imeweka rekodi mpya ya kufikia thamani ya $138 kwa hisa moja katika siku ya jana.

Hii ni kampuni ya kuhakikisha unamiliki hisa zake.

🆕 Google imeanza mpango wa kutumia micro-reactor za nuclear katika kuzalisha umeme wa data center zake.

Mpango huu upo katika mchakato wa kuanza mwaka 2030